KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU CHA 18B KINASEMA,
Katika kutumia haki ya kujilinda mwenyewe au kumtetea mtu mwingine au kutetea mali, mtu atatakiwa tu kutumia nguvu za kiasi zinazostahili ulinzi husika.
Mtu atawajibika kuwa ametenda kosa la jinai kwa kosa lolote litakalotokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda au anapomlinda mtu mwingine au anapolinda mali.
Mtu yeyote atakayesababisha kifo cha mtu mwingine kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda, anakuwa ametenda kosa la kuua bila kukusudia.
Imeandikwa na mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿