⚖️ KUSAMBAZA UJUMBE WA UBAGUZI MTANDAONI — NI KOSA LA JINAI ⚖️
Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kimtandao [Sura ya 443 Toleo la 2023], Kifungu cha 17, ni kosa la jinai kupitia mfumo wa kompyuta:
❌ Kutengeneza au kuchapisha maudhui ya kibaguzi au chuki dhidi ya watu wa rangi, kabila au utaifa fulani.
❌ Kusambaza au kufanya maudhui hayo yapatikane mtandaoni.
❌ Kutuma au kurusha maudhui ya kibaguzi kwa njia ya mtandao.
📌 Adhabu:
Faini isiyopungua Shilingi Milioni 3, au
Kifungo kisichopungua mwaka 1, au vyote kwa pamoja.
📝 Mtandao si sehemu ya kusambaza chuki — sheria ipo.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿