⚖️ JE, MAMA MJAMZITO AU ANAYENYONYESHA ANAWEZA KUPANGWA SHIFT ZA USIKU KAZINI? ⚖️
Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini [Sura ya 366 Toleo la 2023], Kifungu cha 21, kazi ya usiku ni kazi inayofanyika kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 12:00 asubuhi.
📌 Sheria inakataza mwajiri kumlazimisha mfanyakazi kufanya kazi saa za usiku akiwa ni:
👩🍼 Mama mjamzito ndani ya miezi 2 kabla ya kujifungua.
👶 Mama aliyejifungua ndani ya miezi 2 baada ya kujifungua.
🏥 Mfanyakazi aliyethibitishwa na daktari kuwa hafai kufanya kazi za usiku.
✅ Aidha, sheria inalinda afya ya mama na mtoto.
Iwapo mazingira ya kazi ya usiku yanaweza kuhatarisha afya ya mama anayenyonyesha au kumzuia kutekeleza unyonyeshaji ipasavyo, mama anaweza kuwasilisha cheti cha daktari, na mwajiri anatakiwa kumpangia kazi ya mchana pale inapowezekana.
📝 Sheria inalenga kulinda afya, utu na ustawi wa mfanyakazi pamoja na mtoto.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿