Mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa jasho la wanandoa wote wawili hugawanywa sawa kwa kila mmoja. Mchango katika kupatikana kwa mali hizo ndio sababu kubwa ambayo huzingatiwa katika kugawa mali za ndoa.
Mchango katika kupatikana kwa mali za ndoa ni pamoja na kazi za nyumbani ambazo hufanywa na wanawake katika ndoa. kazi hizo hutambuliwa kisheria Kama mchango unaompa haki mwanamke kupata mgao katika mali zilizochumwa pamoja baada ya ndoa kuvunjika.
Mali zinazogawanywa ni zile zilizopatikana kwa nguvu ya pamoja na si mali binafsi za wanandoa waliotengana. Kuna uwezekano kwa wanandoa kuwa na mali binafsi ambazo haziangukii katika mali za ndoa.
#ijuesheria
#sheria
#sheriatanzania
#mwanasheria
#jungulasheria
#sheriahouse

2 Maoni
Kazi mzuri
JibuFutasafi sana
JibuFutaWEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿