Baada ya ndoa kuvunjwa na mahakama, hutolewa amri ya mahakama kuhusu uangalizi na matunzo ya watoto.
Haki ya kuishi na watoto hutegemea umri wa mtoto au watoto, uwezo wa kifedha wa kuwatunza na ustawi wa mtoto mwenyewe.
Mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 7 hupaswa kuishi na mama kwaajili ya ustawi wake kama mtoto, lakini ni lazima ionekane wazi kuwa mama ana tabia njema na ustawi wa mtoto hautaathiriwa.
Mtoto mwenye miaka zaidi ya saba anaruhusiwa kuchagua kuishi na baba au mama. Baba atawajibika kutoa matunzo ya kifedha kadri ya uwezo/kipato chake kama mahakama itakavyoona inafaa.
Endapo mama ana tabia za ulevi uliopindukia, uchangudoa n.k mtoto au watoto wataishi kwa baba kwaajili ya ustawi bora wa watoto.
#ijuesheria
#sheria
#jungulasheria
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿