Ticker

6/recent/ticker-posts

Je, ndugu wa marehemu wanaweza kutoa fedha za marehemu kutoka mitandao ya simu au benki baada ya kifo ya mpendwa wao?

 


✨ Je, ndugu wa marehemu wanaweza kutoa fedha za marehemu kutoka mitandao ya simu au benki baada ya kifo ya mpendwa wao? ✨

Jibu ni ndiyo. Ndugu wa marehemu wanaweza kupata fedha zake zilizobaki kwenye M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa, benki au huduma yoyote nyingine ya kifedha ambako marehemu ameacha fedha zake.

Lakini si kwa kwenda tu ofisini na kudai fedha — lazima kwanza mahakama iwateue kama wasimamizi wa mirathi.

📌 Mchakato ni huu:

1️⃣ Ndugu wanafungua Shauri la mirathi mahakamani

2️⃣ Mahakama inateua msimamizi wa mirathi

3️⃣ Msimamizi anapewa nyaraka za usimamizi

4️⃣ Kwa nyaraka hizo, anaweza kwenda benki au kampuni ya simu kudai fedha za marehemu kisheria

⚠️ Bila nyaraka za mahakama, hakuna taasisi ya kifedha inayoruhusiwa kutoa fedha za marehemu.

Chapisha Maoni

0 Maoni