Ticker

6/recent/ticker-posts

Hakuna fidia inayotolewa kwa ardhi ambayo inatwaliwa ikiwa tupu.

 


📌 Kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Sheria ya Utwaaji Ardhi.

⚠️ Hakuna fidia inayotolewa kwa ardhi ambayo inatwaliwa ikiwa tupu. Fidia hutolewa kuzingatia kiasi ambacho ardhi hiyo imeendelezwa na athari za kiuchumi zitakazojitokeza.

👉🏽 Eneo litahesabika ni tupu hata kama limewekwa uzio, kusawazishwa, kulimwa bila kupandwa mazao ya kudumu, eneo lililowahi kujengwa lakini baadae majengo kubomolewa na kutelekezwa, eneo linatumika kama egesho la magari au kutupa taka n.k

🌾 Kwa ardhi ya vijijini haitachukuliwa kuwa tupu ikiwa ilikuwa ikitumika kwa kilimo 🌱  au malisho 🐄 ndani ya kipindi cha miezi 12 kabla ya kutangazwa kutwaliwa kwaajili ya matumizi ya umma.

Chapisha Maoni

0 Maoni