Dhamana ni kuachiliwa huru kwa mshtakiwa au mtuhumiwa wa kosa fulani, ili kuliwezesha jeshi la polisi kuendelea kukusanya ushahidi wa kupeleka mahakamani. Pia dhamana inampa nafasi mtuhumiwa kuendelea na shughuli zake za kiuchumi, pamoja na kumuwezesha mtuhumiwa kujiandaa na kesi kwa kutafuta wakili au mwanasheria.
Dhamana ni haki ya kila mtu pale anapopata tatizo hasa la uvunjifu wa sheria na kuwekwa chini ya kizuizi yanii polisi.
Dhamana inaweza kuambatana na kiasi cha fedha kitakachosainiwa na mtuhumiwa ili kumlazimu afate masharti ya dhamana bila kuyavunja.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿