Ticker

6/recent/ticker-posts

HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUOMBA TALAKA.



Mtu yeyote anayetaka kuomba talaka mahakamani lazima kufuata taratibu zifuatazo;

Kwanza kabisa kifungu cha 101 kinaeleza kwamba muomba talaka anatakiwa kupeleka malalamiko ya matatizo ya ndoa yake kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa la Kamishina wa Ustawi wa Jamii au baraza lingine linalotambuliwa kisheria kama kanisani au BAKWATA.

Baraza la usuluhishi likishindwa kuwasuluhisha litatoa hati ya kwenda mahakamani. Hati hiyo huandikwa katika fomu maalumu inayoitwa “Fomu Na.3”. Kwa mujibu wa kifungu cha 106(2) madai ya talaka yanatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya miezi sita tangu tarehe baraza la usuluhishi la ndoa lilipotoa hati hiyo. Ni muhimu kufahamu kuwa baraza la usuluhishi la ndoa halina mamlaka ya kutoa talaka au kugawa mali za wanandoa bali kazi yake ni kusuluhisha tu.

Baada ya hapo muomba talaka anatakiwa kutayarisha madai ya kuvunja ndoa na kuyawasilisha mahakamani akiambatanisha vielelezo vyovyote anavyoona vinaweza kuunga mkono madai yake. Kama shauri linafunguliwa mahakama ya mwanzo, basi mhusika anatakiwa kwenda kwenye hiyo mahakama na atapatiwa fomu maalum ambayo atajaza madai yake.


#ijuesheria 

#sheria

#istagram 

Chapisha Maoni

0 Maoni