KIFUNGU CHA 252 CHA SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20 ILIYOREJEWA MWAKA 2019.
Kinasema, Pale inapoonekana kwa hakimu kwamba mtu yeyote ambaye ni mgonjwa sana au kaumizwa sana na inaonekana kwamba hawezi kupona au kwamba kwa sababu zozote zile a naweza asiwepo kutoa ushahidi katika siku ya usikilizaji wa kesi lakini anaweza na yuko tayari kutoa ushahidi wa msingi kuhusiana na kosa, mahakama inaweza kuchukua kwa maandishi maelezo yake kwa kiapo au kwa kuthibitisha na atasaini na kuthibitisha kwamba imebeba maelezo yake ya kweli na hakimu anayechukua maelezo hayo atathibitisha sababu za kuchukua maelezo na ataeleza tarehe na mahali na ni lini na wapi yalipochukuliwa, atatunza maelezo hayo na kuyaweka kwenye faili kwa ajili ya kumbukumbu. Isipokuwa kwamba pale ambapo maelezo ni ya mtu ambaye kwa sababu ya umri wake mdogo au kwa sababu ya imani yake ya kidini hatakiwi kwa maoni ya hakimu kuapa au kuthibitisha, maelezo yanaweza kuchukuliwa bila kiapo au kuthibitisha.
Imeandikwa na
Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿