NI kupokea na kujadili taarifa kuhusu:
• Miradi inayoendeshwa katika eneo la Mtaa na maendeleo yake;
• Hali ya usalama na ulinzi katika eneo la Mtaa;
• Matatizo ya huduma za jamii na hatua zilizochukuliwa;
• Maamuzi ya Kamati ya Maendeleo ya Kata au ya Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji kupitia Kamati ya Maendeleo ya Kata yanayohusu Mtaa;
• Maamuzi ya Kamati ya Mtaa na utekelezaji wake;
• Suala lingine lolote linalohusu utoaji wa huduma na maendeleo ya kijamii na kiuchumi;
• Kumwondoa madarakani Mwenyekiti wa Mtaa inapodhihirika kwamba ameshindwa kumudu madaraka yake kwa kuzingatia sheria.
Sheria Namba 7, 8 na 9 kama zilivyopitishwa na Bunge mwaka 1982 na kurejewa tena mwaka 1999 na 2000, zinatoa muongozo juu ya uendeshaji na usimamizi wa Serikali za Mitaa ikiwemo majukumu yake.
Imeandikwa na Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿