Je unazijua sababu za kunyimwa dhamana kwa makosa yanayodhaminika?
1.Kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana.
Mkosaji anayeshindwa kutekeleza masharti ya dhamana anaweza kukamatwa na kunyimwa dhamana kutokana na kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana.
2. Kama mwomba dhamana ana historia ya uhalifu na kifungo kinachozidi miaka mitatu.
Mtu hawezi kupewa dhamana kama ana historia ya kifungo Cha miaka zaidi ya mitatu ikithibitika kuwa ana rekodi ya uhalifu.
3. Kama Kuna uwezekano wa mtuhumiwa kuruka dhamana au kutoroka.
Kama mtuhumiwa anahisiwa anaweza kutoroka kukimbia mashtaka yake, anaweza kunyimwa dhamana hata Kama kosa alilotenda linadhaminika.
4. Maslahi ya umma/ usalama wa umma na usalama wake mwenyewe mtuhumiwa.
Kama Kuna maslahi ya umma kwa kumnyima mtu dhamana mtu anaweza kunyimwa dhamana, pia Kama mtuhumiwa anaweza kuhatarisha usalama wa raia pamoja na usalama wake anaweza kunyimwa dhamana.
5. Uwezekano wa kuingilia ushahidi.
Kama inaonekana kuwa kumpa mtuhumiwa dhamana itaingilia ushahidi, Basi mtuhumiwa anaweza akakosa dhamana. n.k
Karibu kwa maelezo zaidi: 0758218269.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿