Ticker

6/recent/ticker-posts

UWEZO WA MKURUGENZI WA MASHTAKA KUFUTA MASHTAKA/KESI.




KIFUNGU CHA 91(1) CHA SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI, SURA YA 29 ILIYOREJEWA 2019,  KINASEMA:;


Katika kesi yoyote ya jinai na katika hatua yoyote ile kabla ya hukumu au uamuzi, kama itakavyokuwa, Mkurugenzi wa 

Mashtaka anaweza kufuta kesi aidha kwa kueleza mahakamani au kwa kuiambia mahakama husika kwa maandishi kwa niaba ya Jamhuri kuwa mwenendo hautaendelea;


Na baada ya hapo mtuhumiwa ataachiwa mara moja kuhusiana na shtaka ambalo limefutwa na kama amepelekwa gerezani atatakiwa kuachiwa, au kama yuko chini ya dhamana wadhamini wake watakoma kuwa wadhamini; 


Lakini kuachiwa huko kwa mtuhumiwa hakutachukuliwa kama kizuizi kwa mashtaka mengine ya baadaye dhidi yake kwa kutumia maelezo hayo hayo.


Kifungu kidogo cha pili cha kifungu cha 91 kinaelekeza kwamba, iwapo mtuhumiwa hayupo mbele ya mahakama wakati shtaka lake linafutwa, msajili au karani wa mahakama atatakiwa mara moja kuhakikisha notisi ya maandishi ya kufutwa kwa kesi inapelekwa kwa mtunzaji wa gereza ambamo mtuhumiwa anaweza kuwa anazuiwa na kama mtuhumiwa amepelekwa kwa kusikiliza shauri, kwa mahakama ya chini ambako ndiko alikosikilizwa 

na mahakama hiyo italazimika mara moja kuhakikisha notisi kama hiyo ya maandishi anapewa shahidi yeyote anayewajibika kutoa ushahidi na kwa wadhamini wake (kama wapo) na vilevile kwa mtuhumiwa na wadhamini wake kama alishatolewa kwa dhamana.

Chapisha Maoni

0 Maoni