Ticker

6/recent/ticker-posts

Mamlaka ya mkurugenzi wa mashitaka kufuta mashtaka ya jinai.

 


📜 NOLLE PROSEQUI KATIKA KESI ZA JINAI 🇹🇿⚖️

Katika kesi yoyote ya jinai, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anaweza kuamua kusitisha mashitaka (nolle prosequi) wakati wowote kabla ya hukumu. Hii inaweza kufanyika kwa kutamka mahakamani au kwa kuwasilisha taarifa kwa maandishi.

👉 Mara baada ya uamuzi huo:

✅Mtuhumiwa ataachiliwa huru kwa mashtaka hayo.

✅ Kama alikuwa gerezani, ataachiwa mara moja.

✅Ikiwa alikuwa nje kwa dhamana, dhamana yake itasitishwa.

⚠️ Hata hivyo, kuachiliwa hakuzuii kufunguliwa upya kwa kesi endapo kutapatikana ushahidi wa kutosha.

📌 Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [SURA 20 R.E. 2022], Kifungu cha 91.

#SheriaNaHaki ⚖️ #Tanzania 🇹🇿 #hakikwawote

Chapisha Maoni

0 Maoni