Ticker

6/recent/ticker-posts

SERA YA FARAGHA.

SERA YA FARAGHA

Sera hii ya faragha itahusu watumijia wa Jungulasheria.co.tz pekee, sera ya faragha itahusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kulinda na kuhifadhi taarifa zako wewe mwenyeji wa Jungu la sheria, soma kwa makini sera hii ya faragha kabla ya kuanza kutumia Jungu la sheria ili ujue usalama wa taarifa zako.

JINSI TUNAVYOKUSANYA TAARIFA ZAKO

Tunakusanya taarifa zako binafsi pale unapotembelea, kujisajili, kuweka au kutoa maoni katika tovuti yetu, pia endapo utawasiliana nasi au kutoa mrejesho. Utakapohitaji kutoa maoni katika tovuti yetu au kujisajili au shughuli yoyote katika tovuti yetu utahitajika kuweka jina, barua pepe na ujumbe wako, taarifa tutakazo kusanya kutoka kwako ni JINA, BARUA PEPE, NAMBA YA SIMU na taarifa zingine endapo zitahitajika. 

WAKATI UPI TUNAKUSANYA TAARIFA ZAKO

Tunakusanya taarifa zako binafsi pale tu utakapojisajili Jungulasheria au utakapotufuata kwa kutumia barua pepe yako, taarifa tunazokusanya ni JINA, BARUA PEPE NA NAMBA YA SIMU endapo itahitajika.

TUNATUMIAJE TAARIFA ZAKO

Tunaweza kutumia taarifa tulizokusanya kutoka kwako wakati ulipotembelea, kujisajili, kutoa maoni au mrejesho au kuwasiliana na Jungu la sheria kwa kukupasha habari kuhusu mada mpya zilizoingizwa kwenye tovuti yetu, au kwa kuwasiliana nawe moja kwa moja kukufahamisha kuhusu jambo ambalo ungependa kulifahamu.

KUHUSU VIDUKUZI

Vidukuzi ni faili ndogondogo ambazo huingia katika kivinjari chako kwa lengo la kukuwezesha kupata taarifa ambazo uliwahi kuzitembelea kwa haraka zaidi. Tovuti yetu inatumia vidukuzi hivyo kwa lengo la kujua idadi ya watu waliotembelea tovuti yetu na kusoma tabia ya watu wanaotembelea tovuti yetu ili kuweza kuwapa hasa kile wanachokihitaji.

Unaweza pia kusahihisha kivinjari chako kwa kukifunga kisipokee vidukuzi kutoka katika tovuti mbalimbali au huduma mabalimbali mtandaoni, kwa kufanya hivyo utakuwa umevidhibiti vidukuzi hivyo.

KUTOA TAARIFA ZAKO KWA MTU WA TATU

Jungu la sheria hatutatoa taarifa zako kwenda kwa mtu wa tatu ( mtu wa tatu ni mtu mwingine, taasisi au kampuni mbali ya Jungu la sheria na wewe mtumiaji wake ) bila taarifa maalumu kuja kwako mwenye taarifa, mtu wa tatu hatakua kampuni inayotuhifadhia taarifa zetu kama tovuti, au wafanyakazi wanaohusika na tovuti yetu na watu wa karibu katika uendeshaji wa tovuti hii. Tunalazimika kutoa taarifa zako kwa mujibu wa sheria tu hivyo endapo kutakuwa na matakwa ya kisheria ya kupatikana kwa taarifa zako sisi tutatii sheria.

Hakuna taarifa ambazo zitauzwa, kutangazwa na kusambazwa bila idhini ya mwenye nazo isipokuwa katika kutekeleza matakwa ya kisheria pekee.

VIUNGANISHO KWA MTU WA TATU
 ( mtu wa tatu ni mtu mwingine, taasisi au kampuni mbali ya Jungu la sheria na wewe mtumiaji wake) 

Tunaweza kuweka viunganishi kutoka katika tovuti yetu kwenda kwenye tovuti nyingine au kokote nje ya tovuti yetu, lakini tovuti zote za nje ya tovuti yetu zina sera zao za faragha hivyo utumiaji wa taarifa zako katika tovuti hizo hautafungamana na sera yetu ya faragha hivyo soma sera za kila tovuti unayoitembelea zenye viungo kutoka katika tovuti yetu.

Pia kuna owezekano wa kuwekwa matangazo katika tovuti yetu, matangazo yote yatakuwa yanayoendana na maadili ya kitanzania.

TUNAZINGATIA YAFUATAYO

Ulinzi kwa watoto kutokana na mambo yasiyo na maadili mtandaoni.
Ulinzi wa taarifa binafsi za watumiaji wa Jungu la sheria
Sheria za nchi

Chapisha Maoni

0 Maoni