Ticker

6/recent/ticker-posts

Mambo yanayoambatana na talaka.


FAHAMU MAMBO YANAYOAMBATANA NA TALAKA.

1. Mgawanyo wa Mali

Hili ni jambo linaloambatana na talaka, baada ya ndoa kuvunjika, jambo linalofuata ni mgawanyo wa Mali zilizochumwa kwa jasho la pamoja la wanandoa wanaotengana, kila mmoja atapata mgao wa Mali kutokana na mchango wake katika kupatikana kwa Mali hizo. Hata kazi za nyumbani kwa mwanamke ni mchango katika uzalishaji Mali kwa familia.

Japokuwa ni lazima kuthibitisha kwa ushahidi wa kuaminika kuhusu mchango katika Mali za familia na si kwa maneno ya mdomo.

2. Matunzo ya watoto

Kuvunjika kwa ndoa hakuondoi haki ya watoto kupata matunzo na mahitaji kutoka kwa wazazi, hivyo Basi kwa kuzingatia hali ya kipato Cha wazazi na makuzi pamoja na maendeleo ya mtoto, mahakama itaelekeza ni nani akae na watoto.

Haki ya kuwatembelea watoto kwa mzazi ambae hakukabidhiwa jukumu la kuwalea inabaki pale pale bila kuathiri maendeleo na makuzi ya mtoto.

Rafiki wa faida ni Jungu la sheria, endelea kuwa nasi.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni