Unazijua namna za kupata ardhi nchini TANZANIA?
1. Ardhi ya kutwaa
Njia hii hutumika pale ambapo mtu huingia katika eneo kama vile pori na kusafisha kisha kuliweka katika matumizi. Njia hii ni kongwe sana hapa nchini. Pori linalosafishwa linaweza kuwa ardhi ya kijiji, hifadhi au ya jumla. Ni ngumu kutumia njia hii nyakati hizi, lakini bado inatumika katika maeneo mengi ya Tanzania. Pale ambapo utatakiwa kufuata taratibu kama vile kusajili utatakiwa kutii amri hiyo. Kama utatakiwa kuhama eneo hilo basi mamlaka husika itatakiwa kulipa fidia ya maendelezo uliyoyafanya katika ardhi hiyo.
Hali kadhalika, mtu anaweza kutwaa ardhi kwa kuachwa akae kwenye ardhi au nyumba ya mtu fulani kwa kipindi kirefu kisichopungua miaka kumi na mbili (12) kama vile yuko kwenye ardhi yake na kuweza kufanya kila atakavyo bila kukumbushwa, kukemewa, kulipishwa kodi au bila ya bughudha ya aina yeyote ya umiliki huhesabiwa kuwa anamiliki ardhi ile kihalali. Hata hivyo, njia hii ya utwaaji haiwezi kutumika dhidi ya ardhi inayomilikiwa na taasisi ya serikali.
2. Ardhi ya kurithi
Hii ni ardhi ambayo mrithi hupata kutoka kwa marehemu ambaye alifariki na kuacha wosia kuwa ardhi itakua Mali yake, au hata bila wosia, mrithi anaweza kugaiwa ardhi na msimamizi wa mirathi.
3. Ardhi ya kununua
Pia unaweza kununua ardhi Kama bidhaa zingine, utalipia Kodi stahiki na utamiliki ardhi hiyo kihalali.
4. Ardhi ya kupangiwa na serikali
Mtu anaweza kupata ardhi kwa kugawiwa na Serikali. Anaweza kuomba ardhi katika ardhi ya jumla au ya kijiji. Kamishina akiridhika kwamba umetimiza masharti atakugawia ardhi hiyo. Katika ardhi ya kijiji, serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya kugawa ardhi. Mwanamke akipeleka maombi ya ardhi serikali ya kijiji itayajadili na kuyapeleka Mkutano Mkuu wa Kijiji kuyapitisha. Kama maombi ni chini ya hekta 21 basi Halmashauri ya Kijiji itamgawia ardhi hiyo.
6. Upangishaji
Upangishaji ni njia mojawapo ya kupata ardhi. Tofauti na njia nyingine za upatikanaji wa ardhi, upangishaji unakupatia haki pungufu na yule anayekupangisha. Mmiliki wa ardhi anaweza kumpangisha mtu mwingine kutumia ardhi yake kwa makubaliano maalumu.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿