JE UNAIJUA HATI YA WITO AU SAMANSI?
Hati ya wito au samansi ni taarifa au wito wa kimahakama katika mfumo wa maandishi.
Wito huu huandaliwa kitaalamu na hulenga kutoa taarifa za wito kwa mtu fulani kumtaka kufika mahakamani au kumtaka kutayarisha na kuwasilisha nyaraka fulani za kisheria mahakamani, au kufika mahakamani kutoa ushahidi.
Hati ya wito au samansi inatakiwa kutaja bayana JINA LA MLENGWA WA SAMANSI, TAREHE, MUDA, SAA na MAHALI ambapo maagizo ya samansi yanatakiwa kutimilizwa. Yaani Kama samansi ni kuhusu kuja kutoa ushahidi, ni lazima samansi hiyo iseme bayana, Jina la Mlengwa, tarehe, muda, saa na mahali ambapo Mlengwa ataenda kutoa ushahidi.
Endelea kujifunza nasi, mawasiliano yetu ni mali yako, piga simu kwa maelezo zaidi.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿