Ticker

6/recent/ticker-posts

Je unajua kuhusu masaa ya mfanyakazi kufanya kazi yanayoruhusiwa kisheria.


JE UNAJUA KUHUSU MASAA YA MFANYAKAZI KUFANYA KAZI YANAYORUHUSIWA KISHERIA?

Hii ni kwa waajiri na waajiriwa wote. Kutokana na sheria ya kazi, kifungu namba 19, mwajiri hatakiwi kumtaka au kumruhusu mfanyakazi wake kufanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku.

Mwajiri hatakiwi kumlazimisha mwajiriwa wake kufanya kazi nje ya masaa maalumu ya kazi yaani masaa 12 labda kwa makubaliano maalumu na mfanyakazi huyo atatakiwa kulipwa nyongeza ya mshahara kutokana na masaa ya ziada aliyofanya kazi.

Pamoja na kuwa mfanyakazi anaruhusiwa kufanya kazi masaa ya ziada, lakini masaa hayo ya ziada yasizidi 50 kwa mzunguko wa wiki nne.

Washirikishe rafiki zako kwenye mada hii.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni