Ticker

6/recent/ticker-posts

Likizo ambazo zipo kisheria na kila mfanyakazi anastahili kuzipata.


JE UNAZIJUA LIKIZO AMBAZO ZIPO KISHERIA NA KILA MFANYAKAZI ANATAKIWA KUZIPATA?

1. Likizo ya mwaka.
Hii ni likizo ambayo kila mfanyakazi anatakiwa kuipata kutokana na mzunguko wa likizo wa mwaka, likizo hii ni ya siku 28 na mfanyakazi na mwajiri wake watakubaliana wakati wa likizo hiyo na ni likizo ya malipo.

2. Likizo ya maradhi.
Likizo hii ni ya siku 126 katika mzunguko wa likizo, na likizo hii ina mgawanyiko wa siku 63 za kwanza ambazo mwajiri atamlipa mshahara wote mfanyakazi wake na siku 63 za kipindi cha pili ambazo mwajiri atamlipa mshahara nusu mfanyakazi wake ambaye ni mgonjwa.

Ili mfanyakazi huyo aendelee kulipwa ni lazima aonyeshe cheti cha matibabu.

3. Likizo ya uzazi kwa mwanamke.
Mwanamke anayetarajia kujifungua anatakiwaatoe taarifa kwa mwajiri wake miezi mitatu kabla ya siku ya kujifungua kufika, mwajiri anaweza kutoa likizo wakati wowote ndani ya wiki mbili tangu likizo hiyo kuombwa, likizo hiyo ni ya siku 84 na endapo mama atajifungua watoto zaidi ya mmoja likizo hiyo inaweza kutanuliwa hadi siku 100.

4. Likizo ya uzazi kwa mwanaume.
Ni likizo ndani ya siku saba tangu mtoto kuzaliwa, siku tatu za malipo na siku 4 endapo mtoto au mama atafariki au kuugua.

ONYESHA UPENDO KWA WAFANYA KAZI KWA KUSAMBAZA MADA HII.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

1 Maoni

WEKA MAONI YAKO HAPA.

TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.

KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿