UHAKIKI WA KIMAHAKAMA NI NINI?
(Judicial review) au uhakiki wa kimahakama ni utaratibu uliowekwa kisheria kwa lengo la kuwezesha wananchi kuomba uhakiki wa maamuzi yaliyotolewa na idara za kiserikali ambazo si mahakama lakini zenye mamlaka fulani kisheria kupitisha maamuzi fulani.
Mfano. Mfanyakazi aliyefukuzwa kazi katika idara za serikali, Kama hakuridhishwa na utaratibu mzima uliotumika kumfuta kazi, Basi hapo ndipo sehemu sahihi ya kuomba uhakiki wa kimahakama wa maamuzi yaliyotolewa na TAASISI husika katika kumfuta kazi mtu huyo.
Uhakiki wa kimahakama kazi yake ni kuangalia uhalali wa kisheria wa adhabu iliyotolewa na taasisi za umma kwa MTU husika, pia kuangalia uhalali wa taratibu zilizotumika katika uendeshaji wa kesi nzima mpaka kufikia kumfuta kazi mtu huyo.
Mahakama kuu ndiyo yenye mamlaka ya kufanya uhakiki wa kimahakama wa maamuzi yaliyopitishwa na idara za umma. Uhakiki huu unapogundua makosa, mahakama ina nguvu ya kufuta uamuzi huo, serikali kulazimishwa kutelekeza wajibu fulani, serikali kuzuiwa kuendelea na suala fulani kulinda haki za watu n.k
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿