KANUNI YA ADHABU, SURA YA 16, KIFUNGU 326(4).
WOSIA NI NINI?
Wosia ni nyaraka yenye taarifa kuhusu mali mbalimbali za mtu (aliye hai au marehemu), mgawanyo wa mali hizo, mapendekezo kuhusu wasimamizi wa mirathi na taarifa mbalimbali ambazo huandikwa na MTU wakati wa uhai wake na namna atakavyopenda Mali zake zitumike baada ya kifo chake.
Kwa dhima ya kifungu kilichotajwa juu, kuharibu nyaraka ya wosia endapo mwenye kuiandika yuko hai au amefariki au daftari la kumbukumbu lililoidhinishwa au kutakiwa na sheria kuwekwa kwa ajili ya kuhakikisha au kuweka
kumbukumbu ya hati ya kumiliki mali yoyote, au kuweka kumbukumbu ya vizazi, ubatizo, ndoa, vifo au mazishi, au nakala ya sehemu yoyote ya daftari hiyo ambayo inatakiwa kisheria kupelekwa kwa afisa yeyote wa umma, mkosaji huyo atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka kumi na nne.
#junguupdates

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿