SHERIA YA NDOA, SURA YA 29 KIFUNGU CHA 64(1).
Sheria ya ndoa chini ya kifungu tajwa hapo juu inamruhusu mwanamke ambaye ameolewa katika ndoa halali inayotambulika kisheria, KUKOPA fedha kwa jina la mumewe, au kuibadilisha mali ya mumewe inayohamishika kuwa fedha na kuitumia katika mazingira ya ulazima wa kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya lazima ya mke au watoto halali wa ndoa wa ndoa hiyo.
Katika kukopa fedha au kuuza mali, ulazima wa kufanya hivyo ni lazima uthibitike, na kiwango cha mkopo wa fedha lazima kiendane na kipato cha mume.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿