KIFUNGU CHA 14, MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI KINASEMA;
Afisa polisi anaweza bila ya hati kumkamata:–
(a) mtu yeyote ambaye anafanya uvunjifu wa amani mbele yake;
(b) mtu yeyote ambaye kwa makusudi anamzuia afisa polisi aliye katika utekelezaji wa majukumu yake, au mtu ambaye ametoroka au anajaribu kutoroka kutoka mahabusu halali kisheria;
(c) mtu yeyote ambaye atakutwa na kitu chochote kinachodhaniwa kwa sababu za msingi kuwa ni kitu kilichoibwa au mtu anayedhamiria kutenda kosa kuhusiana na kitu hicho;
(d) mtu yeyote atakayemkuta amelala au kuzurura katika barabara kuu, yadi, bustani au sehemu nyingine wakati wa usiku na ambaye anamdhania kwa sababu za msingi kuwa ametenda kosa au anataka kutenda kosa au ambaye amebeba bila ya ruhusa halali silaha ya hatari au kifaa cha kuvunjia nyumba;
(e) mtu yeyote ambaye ana sababu za msingi za kuamini kuwa hati ya ukamataji imeshatolewa;
(f) mtu yeyote anayemdhania kwa sababu za msingi kuwa amehusika katika kitendo kilichotendeka sehemu yoyote nje ya Tanzania ambacho, kama kingetendeka Tanzania, kingeadhibiwa kama kosa, na ambacho, kwa mujibu wa Sheria ya Kubadilishana Watuhumiwa, au vinginevyo, anawajibika kukamatwa na kuzuiwa Tanzania;
(g) mtu yoyote anayefanya tendo lolote linaloazimia kutusi nembo ya taifa au bendera ya taifa;
(h) mtu yeyote anayemdhania kuwa ni mzururaji.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿