Mahakimu na Majaji wa mahakama za Tanzania hawaruhusiwi kupokea zawadi ambazo zinaweza kutafsiriwa kama rushwa, zawadi ambazo zinaweza kuingilia au kushawishi maamuzi ya mahakama.
Zawadi ambazo zikitolewa kwa watumishi wa mahakama zinaleta picha mbaya kwa heshma ya mahakama na kusababisha umma kupoteza uaminifu kwa mahakama hazitakiwa kupokelewa na watumishi wa mahakama.
Kanuni za maadili chini ya sheria ya usimamizi wa mahakama zinawataka watumishi wa mahakama pamoja na familia zao kutopokea zawadi yoyote ambayo itashawishi uamuzi wa mahakama vinginevyo nje ya utaratibu wa sheria.
Watumishi wa mahakama wanaweza kupokea zawadi iwapo zawadi hizo zitatolewa kwa uwazi na kufahamika na umma, pia zawadi ambazo zitatoka kwa viongozi wa serikali. Zawadi zote hizo zisionyeshe kushawishi au kuingilia maamuzi ya mahakama vinginevyo nje ya utaratibu wa sheria.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿