Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSU MATUMIZI YA PICHA YA RAIS KATIKA OFISI ZA UMMA. Na Johnson Yesaya. LL.B



FAHAMU KUHUSU MATUMIZI YA PICHA YA RAIS KATIKA OFISI ZA UMMA.

Utaratibu wa kutundika picha za viongozi katika ofisi za umma/serikali ulitolewa katika waraka wa watumishi wa serikali Namba. 3 wa mwaka 1985. Pia kifungu Q. 58 cha kanuni za kudumu za utumishi wa umma (standing orders for public service).

Kutokana na mabadiliko ya mwaka 2009 ya kanuni hizo za kudumu za utumishi wa umma, utaratibu wa utundikaji wa picha za viongozi kwa sasa unaelezwa katika kifungu cha Q.21 cha kanuni za kudumu za utumishi wa umma za tarehe 26/06/2009 (General Notice No. 493).

UTARATIBU HUO UNASEMA KAMA IFUATAVYO;

Kifungu Q.21(1), kinasema kuwa "Picha rasmi ya rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, itawekwa ukutani juu ya dawati la mtumishi wa umma katika ofisi zote za serikali".

Q.21(2) kinasema kuwa, "Picha rasmi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano, itawekwa ukutani juu, ikitazamana na picha ya rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Hivyo basi, Kama umewahi kutembelea ofisi za umma, utakuta picha kubwa ya rais aliyeko madarakani juu ukutani nyuma ya mtumishi wa umma na mbele yake utakutana na picha ya Baba wa Taifa letu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kanuni za kudumu za utumishi wa umma zimetengenezwa chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma, SURA 298 marejeo ya mwaka 2019

Chapisha Maoni

0 Maoni