Ticker

6/recent/ticker-posts

UKIJERUHIWA AU KUUAWA NA MNYAMA PORI, UNARUHUSIWA KUOMBA FIDIA (ENDAPO UMEJERUHIWA) AU NDUGU ZAKO KUOMBA FIDIA (ENDAPO UMEUAWA). Na Johnson Yesaya L.LB.




Sheria ya uhifadhi wa wanyama pori katika kifungu cha 69 na 71 kinaeleza utaratibu na namna ambavyo wahanga wa wanyama pori wanavyoweza kushughulikiwa endapo watapata hasara ya mali kama mazao, kujeruhiwa na kuuawa.


The Wildlife Conservation (Dangerous Animals Damage Consolation) Regulations, 2011. Ni kanuni iliyotungwa chini ya sheria ya uhifadhi wa wanyama pori inayofafanua utaratibu mzima wa kufanya maombi ya kulipwa kifuta machozi kutokana na hasara au kuuwawa na wanyama pori.


MTU ambaye amepata hasara ya mali au mazao, au amejeruhiwa, au ndugu wa karibu wa aliyeuawa na mnyama au wanyama pori, anaweza kufanya maombi ya kulipwa kifuta machozi au fidia kwa kufuata utaratibu ufuatao;


1. Kutoa taarifa juu ya tukio kwa mtendaji wa Kijiji ndani ya siku tatu tangu kutokea kwa maafa au tukio.


2. Kufanya maombi ya fidia kwa mkurugenzi wa wanyama pori ndani ya siku saba tangu kutokea kwa tukio, kwa kutumia fomu maalumu zilizotajwa katika kanuni.


3. Maombi hayo yanatakiwa kithibitishwa na afisa wanyama pori, kilimo au mifugo. Pia mtendaji wa Kijiji au kata anaweza kuthibitisha maombi hayo.


Lazima kuwepo na mashahidi wawili wanaotoka katika eneo lilipotokea tukio, na kama tukio ni kujeruhiwa au kuuwawa na mnyama pori, mtaalamu wa afya anatakiwa kuthibitisha maombi hayo.


4. Baada ya hatua zote kukamilika, mkurugenzi wa wanyama pori atajiridhisha na kulipa kifuta machozi au fidia.

Chapisha Maoni

0 Maoni