Ticker

6/recent/ticker-posts

HAKI YA FARAGHA NA USALAMA WA MTU.



IBARA YA 16 YA KATIBA YA TANZANIA.

16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

 (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.

#sheria
#ijuesheria
#sheriahouse
#jungulasheria

Chapisha Maoni

0 Maoni