IBARA YA 17 YA KATIBA YA TANZANIA.
17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya (a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako nakumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtukwenda anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama; au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla aukuhifadhi maslahi fulani mahususi aumaslahi ya sehemu fulani ya umma, kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyohaitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿