Ticker

6/recent/ticker-posts

JE UNAJUA KUWA UBAKAJI UNAWEZA KUTENDEKA NDANI YA NDOA? Na Johnson Yesaya. LL.B.


KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU 130(1),(2)(a).

Katika kueleza ubakaji, sheria inasema, "Ni kosa kwa mtu wa jinsia ya kiume kumbaka msichana au mwanamke ambaye si mke wake, au awe mke wake ambayeametengana nae bila ridhaa yake wakati wa tendo la ndoa.


Mke na mume wanaruhusiwa kutengana kwa wakati fulani bila kuvunja ndoa, wakati wa kutengana watu hawa wawili wanakuwa huru na hawabanwi au kuwajibika kimapenzi dhidi ya wenza wao. Katika kipindi hicho cha kutengana, endapo mwanaume atamlazimisha mke ambaye ametengana nae na kushiriki nae tendo bila ridhaa yake, atakuwa ametenda kosa la ubakaji.


Kutengana ni kuachana kwa wanandoa kwa kipindi fulani kwa mategemeo ya kurudiana baadae, Mara nyingi hutokea kunapokuwa na migogoro ndani ya ndoa hivyo kila mmoja wao huamua watengane kwa muda kutibu tofauti zao.


MAHAKAMA Ina nguvu ya kutenganisha wanandoa lakini pia hata familia za wanandoa zinaweza kutenganisha wanandoa. 🙏🇹🇿


#sheria

#junguattorneys



Chapisha Maoni

0 Maoni