KUTOKANA na sheria za Tanzania, katika JINAI au MADAI, kunapohitajika mahakama kutoa hukumu ndogo au amri ndogo, Basi baada ya amri hiyo kutolewa nafasi ya kukata rufaa huwa haipo. Sheria na maamuzi mbalimbali ya mahakama kuu kuhusu maamuzi madogo ni kuwa, hakuna nafasi ya kukata rufaa kwa maamuzi madogo, rufaa itaruhusiwa endapo maamuzi hayo madogo yanauelekeo wa kuamua kesi kubwa au kesi ya msingi.
HUKUMU ndogo ni Nini? Ni maamuzi madogo katika kesi ya msingi. Maamuzi haya hutolewa katika kuamua mapingamizi ndani ya kesi ya msingi, maamuzi haya hulenga kuweka kesi sawa sawa kwani hutoa miongozo ya mikingamo mbalimbali katika kesi.
#junguupdates
#jungulasheria
#sheria
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿