SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA Tanzania Na. 11 ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 imetamka kosa la “RUSHWA YA NGONO” chini ya kifungu cha 25, kama kinavyobainisha;
“Any person being in a position of power or authority, who in the exercise of his authority, demands or imposes sexual favours or any other favour on any person as a condition for giving employment, a promotion, a right, a privilege or any preferential treatment, commits an offence and shall be liable on conviction to a fine not exceeding five million shillings or to imprisonment for a term not exceeding three years or to both”
Ambapo kwa tafsiri isiyo rasmi kwa kuwa sheria hii haipo katika lugha ya kiswahili, tafsiri yake ni kwamba;
“Mtu yeyote mwenye mamlaka katika kutekeleza majukumu yake anadai, anaweka sharti la ngono au upendeleo mwingine wowote kama kigezo cha kutoa ajira, kupandisha cheo, kutoa haki au upendeleo wowote unaotambulika kisheria atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya faini isiyozidi Milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja”.
Lakini kosa hili limetajwa na linaangukia katika sheria zingine mbali na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa. Kosa la Rushwa ya ngono linaangukia katika sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200 ya sheria za Tanzania, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019. Pia kosa la Rushwa ya ngono linaangukia katika sheria inayoitwa kanuni ya adhabu (Penal Code cap 16). Katika sheria hizi, kosa la Rushwa ya ngono limepewa adhabu tofauti na ile inayotolewa na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
KANUNI YA ADHABU sura ya 16 kifungu cha 130(1) kinasema, “ni kosa kwa mtu wa jinsia ya kiume kumbaka msichana au mwanamke. Kifungu kidogo cha 3(a) cha Kifungu cha 130 kinasema, mtu yeyote atahesabika kuwa amebaka kama- akiwa mtu wa mamlaka, kuchukulia kigezo cha nafasi yake ya mamlaka, na anatenda kosa la kubaka kwa msichana au mwanamke wa mahusiano ya kiofisi au kwa kukosea anamzuia na kumbaka msichana au mwanamke. Kifungu cha 130(3)(a) Cha Kanuni ya adhabu kinatafsiriwa kuwa kutumia mamlaka ya kiofisi kulazimisha na kufanya ngono na MTU kwa lengo la kutoa haki au huduma ni kitendo cha ubakaji.
Mtu yeyote atakayetenda kosa la kubaka kwa Mujibu wa kifungu Cha 131(1) Kanuni ya adhabu, atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha, au kifungo kisichopungua miaka thelathini pamoja na adhabu ya viboko na faini, na atatakiwa kulipa fidia ya kiasi ambacho kitatamkwa na mahakama, kwa mtu ambaye ametendewa kosa hilo na kwa majeraha aliyoyapata. Adhabu huwa tofauti kwa MTU na MTU kutokana na mazingira ya kosa lenyewe au umri wa mhanga wa ubakaji.
SHERIA YA UHUJUMU UCHUMI sura ya 200 inajumuisha makosa ya rushwa kama sehemu ya makosa ya uhujumu uchumi. Maana yake ni kuwa, kosa lililotajwa kwenye Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, tofauti na kosa lililotajwa katika kifungu Cha 15 Cha Sheria ya rushwa, linahesabika Kama sehemu ya makosa ya uhujumu uchumi. Mjumuisho wa Makosa yatokanayo na Sheria ya rushwa kuwa sehemu ya makosa ya uhujumu uchumi unatokana na kifungu Cha 25 (first schedule) ya sheria ya uhujumu uchumi. Kifungu hicho kinasema;
“A person commits an offence under this paragraph who commits any offence under the Prevention and Combating of Corruption Act other than an offence under section 15 of that Act”
Adhabu ya jumla ya makosa ya uhujumu uchumi ni kifungo cha miaka isiyopungua ishirini jela na isiyozidi thelathini. Sheria inasema Kama nyongeza ya kifungu Cha 60(2) Cha Sheria ya uhujumu uchumi kuwa, Kama kosa la uhujumu uchumi lina adhanu nyingine kubwa zaidi katika sheria nyingine, Basi adhabu hiyo kubwa itatolewa na Mahakama.
Kwa muktadha huu, kosa la Rushwa ya ngono linaweza kuhukumiwa kwa adhabu ya kuanzia miaka mitatu mpaka miaka thelathini kutokana na mazingira mbalimbali na sheria itakayotumika kushtaki mtuhumiwa. Lakini pia kosa hili linaweza kuambatana na adhabu ya viboko na faini. Sheria zinazogusa kosa hili ni Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11 ya 2007 kifungu cha 25, Sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200 kifungu 60(2) na 21 (first schedule), na kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu Cha 130(1),(3)(a) na 131.
PAKUA NAKALA HAPA
Imeandikwa na,
Johnson Yesaya Mgelwa
Mwanasheria
Jungu la sheria Tanzania
Mobile: 0758218269/0628729934
E-mail: yesayajohnson@rocketmail.com
Website: www.jungulasheria.com
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿