Ticker

6/recent/ticker-posts

TARATIBU ZA KUMILIKI SILAHA YA KURITHI / SILAHA YA KUNUNUA.



TARATIBU ZA KUMILIKI SILAHA YA KURITHI / SILAHA YA KUNUNUA.

1. LAZIMA UJUE KAMA SILAHA YA KUMILIKI AU KURITHI.

(a) Kama silaha umenunua kwa mtu hivyo silaha hiyo ni ya kurithi.

(b) Kama silaha ni ya kurithi lazima mwenye silaha aandike barua ambayo ataileta kwa kamanda wa polisi wilaya (OCD) ambayo itamtambulisha huyo mtu anayetaka kurithishwa silaha hiyo.

2. IKIWA SILAHA NI YA MAREHEMU (KURITHI SILAHA YA MTU ALIYEFARIKI).

Lazima kuwepo na barua ambayo wazee,ndugu ama wanakijiji waliokaa wakaona huyo mtu anafaa kumiliki silaha hiyo ikiambatanisha na majina ya waliojadili.

3. IKIWA SILAHA NI YA KUNUNUA DUKANI (MPYA).

(a) Anayetaka kumiliki atafika kituo cha polisi na kuchukua fomu”N” akiwa na picha nne.

(b) Atajaza fomu nne akionyesha majina yake,aina ya silaha pamoja na sababu ya kumiliki silaha.

(c) Kama silaha ni ya kurithi atakuja na barua ya muhtasari wa kuonyesha kama wajumbe 

wamemchagua yeye kuwa mmiliki na ataleta risiti kutoka dukani aliponunua silaha.

(d) Ataonyesha barua ya aliyekuwa mmiliki wa silaha ambayo awali ilihakikiwa ”N” kamanda wa polisi wilaya(OCD) kama mwenye silaha yuko hai.

(e) Akishajaza fomu”N” ambayo itakuwa fomu ya nne ataenda nazo kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya Kijiji na kujadiliwa huko na ataandikiwa muhuktasari.

(f) Ataenda katika kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya Kata pia watamjadili na kumpatia mukhtasari.

(g) Ataenda ngazi ya Tarafa yaani kwenye kamati ya ulinzi na usalama na Katika kamati zote hizo muhuktasari utaonyesha majina ya wajumbe waliomjadili baada ya hapo ataenda kwa hakimu wa Mahakama ya mwanzo ambaye atasaini na kugonga muhuri.

(h) Akimaliza hapo viambatanisho vyake vyote vitafungwa kwa pamoja na kupelekwa kwa afisa usalama wa Taifa wilaya(DSO)ili avihakiki na kutoa makosa yaliyopo kasha kuzirudisha kwa OCD.

(i) Na OCD atachukua viambatanisho vyake vyote kutoka ngazi mbalimbali za Kijiji,Kata,Tarafa na Mahakamani atazipeleka katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na kumjadili kama anastahili ama laa kasha watamuita katika kamati hiyo na maombi yake yatapelekwa Mkoani.

Chapisha Maoni

0 Maoni