Ticker

6/recent/ticker-posts

HAKI YA KUJILINDA

 


KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU CHA 18A.

Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii kila mtu anayo haki ya:-

kujilinda yeye binafsi au mtu mwingine dhidi ya kitendo chochote kinyume cha kisheria au shambulio au utumiaji nguvu dhidi ya mwili; au kulinda mali yake au mali yoyote iliyo chini ya umiliki wake, himaya yake, au chini ya uangalizi wake au mali ya mtu mwingine yeyote dhidi ya kuchukuliwa isivyo halali au kuharibiwa au kufanyiwa fujo.

Katika kifungu hiki, neno "mali ya mtu mwingine yeyote " itajumuisha mali yeyote inayomilikiwa na Serikali au Shirika la Umma au ya mwajiri au mali inayomilikiwa kwa pamoja.


Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )

Wa Jungu la sheria Tanzania

0758218269/0628729934

Chapisha Maoni

0 Maoni