Ticker

6/recent/ticker-posts

KUHATARISHA USALAMA WA VYOMBO VYA ANGA MIAKA "30" JELA.

 


KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU CHA 318A KINASEMA;

Mtu yeyote ambaye- 

anafanya kitendo cha kutumia nguvu dhidi ya mtu aliyeko ndani ya ndege inayoruka kama kitendo hicho kina uwezekano wa kuhatarisha usalama wa ndege hiyo;

anaharibu ndege wakati wa matengenezo au anasababisha madhara kwenye ndege hiyo ambapo inaifanya ishindwe kuruka au kuna uwezekano wa kuhatarisha usalama wakati wa kuruka;

anaweka au anasabisha kuwekwa katika ndege wakati wa matengenezo, kwa njia yoyote iwayo, kifaa au kitu chochote ambacho kina uwezekano wa kuharibu ndege hiyo au kusababisha uharibifu kwenye ndege hiyo au ambayo ingeweza kuifanya ishidwe kuruka au kusababisha madhara kwenye ndege hiyo ambapo kuna uwezekano wa kuhatarisha usalama wakati wa kuruka;

anaharibu au anasabisha madhara vyombo vya kuongozea angani au anaingilia utendaji wa vyombo hivyo, iwapo kitendo chochote kama hicho kina uwezekano wa kuhatarisha usalama wa ndege wakati wa kuruka; au

anatoa taarifa ambayo anajua ni ya uongo, na kuhatarisha usalama wa ndege kwenye kuruka, atakuwa anatenda kosa kosa na anawajibika kuhukumiwa kifungo kisichozidi miaka thelathini pamoja na adhabu ya viboko.

Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)

Wa Jungu la sheria Tanzania

0758218269/0628729934

Chapisha Maoni

0 Maoni