KATIBA YA TANZANIA IBARA YA 46 INASEMA.
Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla aubaada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.
Imeandikwa na mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿