KWA MUJIBU WA SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 2009 ILIYOREKEBISWA 2019, KIFUNGU CHA 8(1);
Kila mzazi au mlezi, ana wajibu wa lazima wa kuhakikisha mtoto anapata haki ya;
1. Chakula
2. Malazi
3. Mavazi
4. Huduma za afya na chanjo
5. Elimu
6. Uhuru na haki ya michezo.
Haitakiwi KUMNYIMA mtoto haki yoyote katika ya hizo tajwa hapo juu. Adhabu ya makosa yatokanayo na kumnyima mtoto haki za msingi ni adhabu ya faini isiyozidi Milioni 5 au kifungo cha miezi 6 jela au vyote kwa pamoja.
Imeandikwa na mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿