Mke halazimiki kumtolea ushahidi mume
Sheria ya ushahidi kifungu cha 130(1) kinasema, 𝒎𝒌𝒆 𝒉𝒂𝒍𝒂𝒛𝒊𝒎𝒊𝒌𝒊 𝒌𝒖𝒎𝒕𝒐𝒍𝒆𝒂 𝒎𝒖𝒎𝒆 𝒘𝒂𝒌𝒆 𝒖𝒔𝒉𝒂𝒉𝒊𝒅𝒊 𝒑𝒂𝒍𝒆 𝒎𝒖𝒎𝒆 𝒉𝒖𝒚𝒐 𝒂𝒏𝒂𝒑𝒐𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒂𝒎𝒆𝒔𝒉𝒕𝒂𝒌𝒊𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒎𝒕𝒖 𝒎𝒘𝒊𝒏𝒈𝒊𝒏𝒆 𝒎𝒂𝒉𝒂𝒌𝒂𝒎𝒂𝒏𝒊. Vilevile, mume halazimiki kumtolea mke ushahidi.
Ushahidi unaolengwa hapa ni ule wa upande wa mashtaka, unaosaidia upande wa MASHTAKA kumtia hatiani mke au mume huyo hatalazimika kutoa ushahidi wowote wa namna hiyo.
Lakini anaruhusiwa/kulazimika kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kumsaidia mume/mke wake asiingie hatiani.
Na akitakiwa kuwa shahidi wa kumfunga/kumtia hatiani mke/mume hapo halazimiki kuja kutoa ushahidi. Hapo juu tumeona kuwa ukitakiwa na mahakama kuja kutoa ushahidi ni lazima kufanya hivyo la sivyo utakuwa umetenda kosa.
Lakini haitakuwa lazima kuja kutoa ushahidi ikiwa mke au mume ameitwa kutoa ushahidi wa kumfunga mwenza, yaani ushahidi unaousaidia upande wa mashtaka. Na hakutakuwa na kosa ikiwa atakataa.
Ila kama mke au mume atahitajika kuja kutoa ushahidi wa kumtetea mwenza asifungwe, yaani ushahidi upande wa utetezi, hiyo ni lazima kuja na asipokuja ni kosa.
Pamoja na hayo hapo juu, mume/mke wanalazimika kutoleana ushahidi wa kufungana ikiwa makosa yaliyotendwa ni:
(a) Yale yaliyo kwenye Sheria ya Ndoa.
(b) Yale yaliyo sehemu ya 15 ya Kanuni za Adhabu, ambayo ni makosa dhidi ya maadili, mfano kubaka, kulawiti, kunajisi nk.
(c) Yale ambayo mke amemshtaki mume wake mwenyewe, au mume amemshtaki mke wake mwenyewe.
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿