DHANA hii haina ukweli wowote, siku huhesabiwa kawaida yaani saa 24.
Sheria ya magereza ya mwaka 1967, kifungu cha 49 kinatoa punguzo la adhabu ya mfungwa kufikia 1/3 ya adhabu yake. Yaani mfungwa yeyote anayeingia jela, anapata punguzo la moja ya tatu ya adhabu yake, Kisha anaendelea kutumikia kipindi kilichobaki.
LAKINI, punguzo la adhabu ya kifungo linakatazwa kwa baadhi ya wafungwa waliofungwa maisha jela na wale waliohukumiwa kunyongwa.
Lakini pia, punguzo hili linaweza kuathiriwa na nidhamu ya mfungwa, endapo baada ya punguzo la adhabu, mfungwa akawa mtovu wa nidhamu gerezani na kujihusisha na uhalifu mbalimbali gerezani ikiwemo kujaribu kutoroka au kutorosha wafungwa wengine, punguzo litafutwa na atatakiwa kutumikia kifungo muda wote anaotakiwa kutumikia.
UFAFANUZI KUHUSU 1/3 YA ADHABU.
Moja ya tatu katika adhabu mfano ni MTU aliyehukumiwa miaka 10 jela, moja ya tatu ni punguzo la miaka 3 kati ya miaka kumi, aliyehukumiwa miaka 20 punguzo ni miaka 6, na aliyehukumiwa miaka 30 punguzo ni miaka 10.
Imeandikwa na Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿