UNAFAHAMU?
Je Unafahamu kwamba kutishia kuua mtu au kutishia kujeruhi kwa kupiga risasi mtu, au tishio la kuchoma au kuharibu mali za mtu ni kosa la jinai?
Kifungu cha 89 kifungu kidogo cha 2(a) na (b) cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyorekebishwa mwaka 2019 vinaeleza kuwa, kutishia kuua mtu au kutishia kujeruhi kwa kupiga risasi mtu, au tishio la kuchoma au kuharibu mali za mtu ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela bila faini.
Kosa hilo hilo linapofanywa wakati wa usiku, Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili jela.
#elimikasheria
Jungu la sheria Tanzania

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿