Rafiki yangu amekamatwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake ili aweze kuomba dhamana mbele ya mahakama, je! Atafanyiwa kama wafungwa wengine awapo mahabusu ukizingatia bado hajahukumiwa?.
JIBU NI HAPANA.
Sheria ya magereza katika kifungu cha 76 inasema, mahabusu watatenganishwa na wafungwa kadri vile itakavyofaa/kuwezekana.
Kifungu cha 77 kinaongeza kwa kusema, mahabusu ambaye si mfungwa, atapata nafasi ya kula vyakula na kunywa vinywaji atakavyopendelea na anaruhusiwa kununua vitu hivyo na mahitaji mengine kama nguo na mashuka mahala popote ndani au nje ya gereza kadri itakavyowezekana.
ANGALIZO : Sheria inazuia kabisa mahabusu kugawa au kuuza vyakula, vinywaji au vifaa ambavyo hawaruhusiwi kuwa navyo wafungwa.
#maswalinamajibu
Jungu la sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿