Ticker

6/recent/ticker-posts

MUHTASARI WA KIKAO CHA FAMILIA NA NDUGU WA MAREHEMU.



Muhtasari ni nakala iliyoandikwa yenye ajenda mbalimbali zilizoongelewa katika kikao cha familia au ukoo baada ya kuhitimisha msiba au mazishi.


Muhtasari huwa na ajenda mbalimbali ikiwemo;


1. Kufungua kikao

2. Kumchagua Mwenyekiti na Katibu wa Kikao.

3. Kusoma wosia aliouacha marehemu Kama upo.

4. Kuainisha/Kutaja Mali Zilizoachwa na Marehemu.

5. Kumteua Msimamizi wa Mirathi.

6. Mengineyo.

7. Kufunga Kikao.


Muhtasari pia unatakiwa uwe na orodha ya wanafamilia au wanaukoo walioshiriki Kikao hicho, majina yao, anuani kama zipo, namba za simu na saini zao.


Muhtasari huu ni muhimu sana kwani hutumika katika kufungua mirathi katika mahakama ambapo marehemu alifia.


Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)

Wa Jungu la sheria Tanzania

0758218269/0628729934.


Chapisha Maoni

0 Maoni