Kwa MUJIBU wa kifungu cha 17 cha sheria ya kudhibiti madawa ya kulevya, ni kosa la jinai kukutwa na dawa za kulevya bila kujali ni zako au ni za mtu mwingine. Kosa hili adhabu yake huanzia kifungo cha miaka 5 mpaka maisha kutegemea na kiasi au uzito wa dawa zilizopatikana. Ifahamike kwamba, baadhi ya makosa ya madawa ya kulevya yanaangukia katika sheria ya makosa ya uhujumu uchumi yasiyo na dhamana.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿