MDAIWA ANAPASWA KULIPWA POSHO NA MDAI ANAPOWEKWA KIZUIZINI KUTOKANA NA MAOMBI YA MDAI
Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Kesi/Mashauri ya Madai, SURA 33 kanuni ya XXI (28, 29, 35 na 38).
Kuna namna nyingi zinazotumika kutekeleza hukumu katika mashauri ya madai. Kukamata na kuuza Mali za mdaiwa ni namna moja, lakini kumuweke kizuizini mdaiwa katika kesi ya madai pia ni namna nyingine inaposhindikana namna ya kwanza hapo juu.
Maelezo yetu yatajikita zaidi katika namna ya pili, kuhusu kumuweka kizuizini mdaiwa wa madai.
Baada ya mahakama kuamua kuwa mdaiwa anatakiwa kulipa kiasi fulani cha fedha kama hukumu, au fidia kwa mdai, mdai anaweza kuiomba mahakama kutoa amri ya kukamata na kuuza mali za mdaiwa, lakini endapo itashindikana kwasababu za mdaiwa kutokuwa na mali yeyote.
Mdai anaweza kuiomba mahakama kukamatwa na kuwekwa kizuizini mdaiwa ambaye ameshindwa kulipa kiwango cha fedha kama hukumu au fidia kwa mdai.
Mahakama ikijiridhisha, na kupanga kiwango cha posho ambacho atalipwa mdaiwa muda wote akiwa kizuizini, Basi mahakama itatoa amri ya kuwekwa kizuizini kwa mdaiwa (mfungwa wa madai) ambapo muda wa kukaa kizuizini haupaswi kuzidi miezi sita.
Mdai atawajibika kumhudumia mdaiwa, na kumlipa posho kila mwezi na mengineyo kama itakavyoamuriwa na mahakama.
Jungu la sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿