Vitisho vya Vurugu na Uharibifu wa Mali 💣🔥🔫
Kwa mujibu wa Kifungu cha 89(2) cha Kanuni ya Adhabu, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote ambaye kwa nia ya kumtisha au kumchokoza mtu mwingine:
🔹 Anatishia kumpiga, kumpiga risasi, kumuua mtu au kuharibu mali yake.
🔹 Anarusha risasi au kufanya kitendo kingine chochote cha kuvuruga amani kwa nia ya kumtia mtu hofu.
⚠️ Adhabu: Kifungo cha mwaka mmoja, na kama kosa litafanyika usiku, adhabu ni kifungo cha miaka miwili.
🛡️ Sheria inalenga kudhibiti vitisho na matendo ya fujo yanayovunja amani na kuhatarisha usalama wa watu na mali.
#VuruguNiKosa #SheriaZaAdhabu #AmaniKwanza #JunguLaSheria 🇹🇿

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿