Ticker

6/recent/ticker-posts

UTARATIBU WA ADHABU YA VIBOKO SHULENI.



UTARATIBU WA ADHABU YA VIBOKO SHULENI.


ADHABU YA VIBOKO shuleni ni suala lenye utaratibu uliowekwa katika Waraka wa Elimu (Na.24) wa mwaka 2002. Waraka huo unaeleza utaratibu mzima wa utoaji adhabu ya VIBOKO kwa kuzingatia ukubwa wa kosa, jinsia, umri na afya ya mtoto.


 Mwalimu MKUU ndiye mwenye mamlaka ya kutoa adhabu hiyo au Mwalimu yeyote mwingine kwa ruhusa ya maandishi kutoka kwa Mwalimu MKUU.


Adhabu ya viboko haipaswi kuzidi viboko vinne na adhabu hii itatolewa tu pale ambapo mwanafunzi amefanya makosa makubwa ya utovu wa nidhamu au makosa ambayo yanaweza kuathiri heshma au hadhi ya shule.


#sherianatehama

#sheria

Chapisha Maoni

0 Maoni