⚖️ NI KOSA LA JINAI KUPIGA PICHA MIILI YA MAREHEMU BILA RUHUSA MAALUMU 🇹🇿
Kwa mujibu wa Kifungu cha 162 cha Kanuni ya Adhabu [SURA YA 16 R.E. 2022], ni kosa la jinai kupiga au kusambaza picha, video au taswira za miili ya marehemu, waathiriwa wa uhalifu au matukio ya kutisha bila idhini.
🚫 Ni marufuku:
❌ Kupiga picha au video za miili ya marehemu au waathiriwa wa uhalifu.
❌ Kusambaza picha hizo kupitia mitandao ya kijamii au njia nyingine yoyote bila ruhusa.
✅ Inaruhusiwa kupiga picha au video kwa sababu zifuatazo tu:
✔️ Uchunguzi wa kihalifu.
✔️ Shughuli za mazishi kwa miili ya marehemu.
✔️ Sababu nyingine zilizoidhinishwa na polisi au mamlaka husika.
⚠️ Adhabu:
Mtu atakayekiuka kifungu hiki anaweza kutozwa faini ya sio chini ya Tsh 1,000,000 au kifungo cha sio chini ya mwaka mmoja, au vyote kwa pamoja.
🔹 Tafakari kabla ya kupiga na kutuma picha za merehemu mitandaoni!
#SheriaNaHaki ⚖️ #Tanzania 🇹🇿 #UsalamaMtandaoni #HakiZaFaragha

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿