⚖️ MAKOSA KUHUSU USAJILI WA WAPIGA KURA 🇹🇿
Kwa mujibu wa Kifungu cha 114 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Sura no. 1 of 2024, mtu yeyote anayehusika katika udanganyifu wa usajili wa wapiga kura anafanya kosa la jinai.
🚫 Makosa yanayohusiana na usajili wa wapiga kura:
❌ Kutoa taarifa za uongo ili kujisajili au kumsajili mtu mwingine.
❌ Kujisajili mara mbili katika vituo tofauti bila kufuata taratibu.
❌ Kuomba upya kadi ya mpiga kura kwa njia ya udanganyifu.
❌ Kununua, kuuza, kuiba au kuharibu kadi ya mpiga kura kwa lengo la kuzuia mtu kupiga kura au kuongeza kura kwa mgombea fulani.
❌ Kumzuia au kumkwamisha afisa wa uchaguzi katika kutekeleza majukumu yake.
⚠️ Adhabu:
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia anaweza kutozwa faini kati ya TZS 100,000 hadi 300,000 au kifungo cha miezi 6 hadi miaka 2, au vyote kwa pamoja.
🔹 Kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki ni wajibu wa kila mmoja. Epuka vitendo vya udanganyifu!
#SheriaNaHaki ⚖️ #Tanzania 🇹🇿 #UchaguziHuru

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿