WIZI WA KUAMINIKA NI KOSA LA JINAI 🇹🇿
Kwa mujibu wa Kifungu cha 273 cha Kanuni ya Adhabu [SURA YA 16 R.E. 2022], mtu yeyote anayepokea mali kwa misingi ya uaminifu kama wakala, msimamizi, au mtu mwenye mamlaka ya kuihifadhi au kuitumia kwa manufaa ya mtu mwingine, na kisha akaiba mali hiyo, anafanya kosa la jinai.
🚫 Vitendo vinavyoweza kuwa kosa:
❌ Wakala au mtu mwenye power of attorney akitumia mali kinyume na makubaliano.
❌ Mtu anayepewa mali kwa usimamizi halafu akaiba au kuitumia kwa manufaa yake binafsi.
❌ Kupokea pesa au mali kwa niaba ya mtu mwingine na kuzitumia isivyo halali.
⚠️ Adhabu:
Mtu atakayepatikana na hatia anaweza kufungwa hadi miaka 10.
🔹 Uaminifu ni msingi wa haki! Usitumie vibaya mali ya mtu mwingine.
#SheriaNaHaki ⚖️ #Tanzania 🇹🇿 #Uwajibikaji #AminiwaUsisaliti

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿