Ticker

6/recent/ticker-posts

Kudharau Mahakama Kosa la Jinai.



Kudharau Mahakama kosa la Jinai ⚖️

Kwa mujibu wa Kifungu cha 114 cha Kanuni ya Adhabu, mtu yeyote anayefanya jambo lolote linalodharau au kuharibu heshima ya Mahakama au kuathiri mwenendo wa kesi, anakuwa ametenda kosa la kudharau mahakama.

🚫 Vitendo vinavyohesabika kama Kudharau Mahakama ni pamoja na:

🔹 Kuonyesha dharau kwa maneno au matendo ndani ya ukumbi wa Mahakama.

🔹 Kukataa kuapa au kutoa ushahidi baada ya kuitwa kama shahidi.

🔹 Kusababisha fujo au kero wakati wa mwenendo wa kesi.

🔹 Kuchapisha au kusema habari zinazopotosha au zinazoathiri mwelekeo wa kesi.

🔹 Kuchapisha ushahidi wa kesi ya faragha.

🔹 Kuingilia au kushawishi shahidi kutoa ushahidi kwa njia isiyo halali.

🔹 Kumfuta kazi mfanyakazi kwa sababu ya kutoa ushahidi mahakamani.

🔹 Kuchukua tena mali au mtoto ambaye Mahakama imetoa uamuzi kuhusu umiliki au uangalizi wake.

🔹 Kukataa kulipa fidia au gharama kama ilivyoamuliwa na Mahakama.

🔹 Kufanya tendo lolote la makusudi la kudharau Mahakama au mwenendo wa kesi.

⚖️ Adhabu:

Kifungo cha hadi miezi sita au faini isiyozidi shilingi 100,000.

👉 Ikiwa kosa limefanyika mbele ya Mahakama, jaji au hakimu anaweza kumhukumu mhalifu siku hiyo hiyo kwa faini ya shilingi 400 au kifungo cha hadi miezi sita.

🔍 NB: Hii ni tofauti na mamlaka ya Mahakama Kuu katika kushughulikia makosa ya dharau.

#SheriaZaTanzania #ContemptOfCourt #HeshimaKwaMahakama #JunguLaSheria ⚖️

Chapisha Maoni

0 Maoni